Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga imeziasa Taasisi binafsi, Makampuni, Asasi za Kiraia na watu binafsi kushirikiana na katika kutatua changamoto zinazokabili makazi ya wazee na watu wenye ulemavu nchini. 

Akiongea wakati alipotembelea Makazi ya kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga Bi. Sihaba amesema kuwa ametembelea baadhi ya makazi hayo na kuona yanahitaji msaada mkubwa hasa ujenzi wa nyumba za malazi, umeme na madawa hivyo Taasisi binafsi, Makampuni, Asasi za Kiraia na watu binafsi hawana budi kushirikiana na serikali kamaliza kabisa changamoto hizo.

“nimetembelea makazi kadhaa sasa, changamoto ni nyingi, wazee hawa wanahitaji msaada mkubwa sana hivyo kwa nafasi hii natoa wito kwa Taasisi binafsi, Makampuni, Asasi za Kiraia na watu binafsi kushirikiana na serikali katika kuziondoa changamoto hizi katika makazi haya ili kuweza kuwafanya wazee hawa kufurahia maisha katika makazi haya”.Amesema Bi. Sihaba.

Naye Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe amewaomba wahisani na serikali kwa ujumla kusaidia katika ukarabati na ujenzi wa majengo katika makazi hayo ili kupunguza changamoto ikiwemo uvamizi wa vijana wanaotumia vilevi na bangi kuingia katika nyumba hizo na kutishia kuwafanyia vitendo vibaya wazee wenye jinsia ya kike.

Akizungumza kwa niaba ya Wazee katika Makazi ya Kolandoto Mkoani Shinyanga Mzee Samora Maganga amesema kuwa kituo hicho kwa kiasi fulani kipo katika hali nzuri ila wanaiomba serikali iwasaidie katika kutatua changamoto ya umeme na majengo kwani imekuwa kero ya muda mrefu sasa.

Aidha Bi. Sihaba akiongea na Wazee katika Makazi ya Amani Mkoani Tabora aliwapongeza walezi wa makazi hayo kwa kuamua kutoa kadi za matibabu za CHF kwa wazee hao na kushauri Walezi wa Makazi mengine ya Wazee nchini kuiga mfano huo ili kusaidia katika utoaji bora wa huduma za afya kwa wazee.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Wazee wanaoishi katika Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga na kuwahakikishia serikali kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ili kuwawezesha kuishi katika mazingira rafiki. Katikati ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara hiyo Bi. Amina… na kushoto ni Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe.
Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga sehemu ya nyumba zinazohitaji ujenzi kwa ajili ya Makazi ya Wazee hao. Wakati wa Ziara ya Kutembelea Makazi ya Wazee na kuona hali halisi ya makazi hao.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Wazee katika Makazi ya Kulea Wazee ya Amani leo Mkoani Tabora.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...