Mkurugenzi Mtendaji wa NMB,  Ineke Bussemarker akizungumza katika uzinduzi mpango wakuwawezesha watoto na vijana kujua umuhimu wa kutumia taasisi za fedha katika kutunza na kujiwekea akiba kwaajili ya matumizi ya baadae katika shule ya msingi Mlimani leo jijini Dar es Salaam.  
  Mchekeshaji Lucas Mhavile (Joti) akichekesha katika uzinduzi mpango wakuwawezesha watoto na vijana kujua umuhimu wa kutumia taasisi za fedha katika kutunza na kujiwekea akiba kwaajili ya matumizi ya baadae katika shule ya msingi Mlimani leo jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dk.Edicome Shirima akikata utepe kuashiria uzinduzi mpango wakuwawezesha watoto na vijana kujua umuhimu wa kutumia taasisi za fedha katika kutunza na kujiwekea akiba kwaajili ya matumizi ya baadae katika shule ya msingi Mlimani leo jijini Dar es Salaam. 

Na Mwandishi Wetu.
Benki ya NMB kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Women's World Banking wamezindua mpango wakuwawezesha watoto na vijana kujua umuhimu wa kutumia taasisi za  fedha katika kutunza na kujiwekea akiba kwaajili ya matumizi ya baadae. 

Akizungumza na  kwenye uzinduzi wa WAJIBU, Mkurugenzi wa Elimu wa Wizara ya  Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dk.Edicome Shirima alisema “Walaji wenye uwezo, wanaojiamini na walioshirikishwa wanaofanya maamuzi sahihi ya kifedha si tu ataboresha maisha yao bali jamii kwa ujumla. Ninafarijika sana leo kuzindua mpango huu wa WAJIBU kwani
nina Imani kuwa utasaidia kuwapatia watoto na wazazi stadi muhimu zitakazowawezesha kupanga maisha
yao ya baadae.”

Amesema serikali imedhamiria kwa dhati kabisa kuboresha na kuendeleza elimu ya fedha katika ngazi
zote za watanzania – Hususani wanajamii yote ya Tanzania,

Shirima  amesema mpango  huo wa jifunze, Jipange – WAJIBIKA inajumuisha vipindi vitatu kwa ajili ya shule za sekondari na msingi –Kipindi cha kwanza  kitazingatia mafunzo ya elimu ya masuala ya fedha na taasisi za kifedha itakayowaunganisha wanafunzi na wazazi wao, na kufuatiwa na vipindi viwili maalumu kwa watoto wenyewe katika mafunzo hayo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa NMB,  Ineke Bussemarker amesema kuwa mpango huo umepewa jina la WAJIBU mahususi kwaajili ya akaunti za akiba za watoto na vijana,WAJIBU yenye maana ‘Wajibika’ inajumuisha aina tatu za akaunti za akiba ambazo ni  NMB Mtoto Akaunti, NMB  Chipukizi Akaunti na NMB Mwanachuo Akaunti zilizotengenezwa kwaajili ya vijana katika kila hatua ya maisha.

Bussemarker amesema kuwa  upatikanaji wa huduma za kifedha na uelewa wa kuzitumia kwa vijana itaisaidia benki ya NMB  kutimiza azma ya kujenga utamaduni wa kuhifadhi fedha kwa matumizi ya baadae.

Amesema kuwa si tu kwa kuwekeza na kuwa na jamii ya vijana yenye uelewa wa  masuala ya fedha tangu wakiwa wadogo bali inaleta tija kwa biashara pia. WAJIBU ni fursa kwa wafanyakazi changia kwa jamii huku wakiisaidia benki kufikia soko jipya la vijana wanaoweka akiba benki.

Bussemarker  amesema kuwa  WWB kuandaa mpango kazi wa WAJIBU, NMB imefaidika kutokana na uzoefu wa miaka 
zaidi ya 35 ya taasisi ya kimataifa ambayo imefanya tafiti za kina za kuelewa tabia na uwezo wa kifedha wa 
wanawake na wasichana na maisha yanayosababisha tabia hizo. 

Mkurugenzi wa Bidhaa wa WWB, Jennifer McDonald amesema amefarijika sana kushirikiana na NMB ushirikiano ambao umewaletea wananchi mpango wetu wa WAJIBU,kama tunavyojua kuwa na akaunti za akiba ni hatua moja tu,” alisema 

“Ndiyo maana tunawapongeza NMB kwa kupanua zaidi WAJIBU kwa kuingiza vipengere vya mpango wa kuelimisha jamii kuhusu masuala ya kifedha itakayo wajengea uwezo vijana na kuwawezesha kuwa na maarifa
na nguvu ya kutumia akaunti za akiba vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...