Waliosimama kutokujibu kushoto Mapunda, Hassan Shariff (Mhabeshi), Jaffari Kajembe, Dr Ramadhani Dau, na Kassim Manara. Walioketi kutokujibu kushoto Mohamed Yahaya Tostao, Mohamed Mkweche, Jafari AbdulRahaman, Beda Simtaji na Gordian Mapango. Picha imepigwa jana  Ijumaa Juni 22, 2012 katika klabu  ya Pan Africa mtaa wa Swahili ikiwa kama kumbukumbu ya  mchezaji Kassim Manara   nchini baada ya  miaka takriban 25 toka aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2012

    MUNGU AMJALIE DR DAU MAISHA MAREFU NA YENYE AFYA NJEMA.
    MTU MZITO KAMA YEYE KUWA KARIBU NA WATU WA KAWAIDA KAWA HAWA INAHITAJI KUJIAMBUA KULIKO KAWAIDA .
    DR DAU UNASTAHILI KUWA RAIS WA NCHI HII.

    MWANA DAR

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2012

    PICHA HAINA USHIRIKIANO, KUNA AINA NYINGI ZA PICHA KUNA AMBAZO NI ZA MATUKIO MBALIMBALI HAPO MTU ANAPIGA PICHA TOFAUTITOFAUTI LAKINI HII NI PICHA YA KUMBUKUMBU NILITEGEMEA WAPIGWAJI WANGEONYESHA USHIRIKIANO KWA POZI ZURI MAANA HUYU ANASOMA SMS NA HUYU AMEANGALIA HUKU ILIMRADI TU, MICHUZI INGILIA KATI NENDA KAPIGE PICHA MWENYEWE UMPATIE MANARA KWA KUMBUKUMBU NZURI

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2012

    Wewe Mdau uleyesema Dr Dau ni mtu mzito na amekaa na watu wa kawaida, acha ugagagigikoko. Dau ni mtoto wa magomeni mapipa. Ndipo alipozaliwa na ndipo alipolelewa na kukulia. Hao unaowaona naye hapo ndiyo ma-homeboys wake kwa hiyo yeye mwenyewe wala hajioni kwamba yeye ni mtu muhimu kuliko wengine.

    ReplyDelete
  4. picha nzuri sana ni moja ya kumbukumbu nzuri na ya kujivunia,hongera dr dau

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 23, 2012

    Na wewe unaesema Dau ni mtoto wa magomeni Mapipa hujui ulisemalo. Dau kazaliwa Kariakoo (Fire) kakulia hapo na kasoma Aga Khan (Muhimbili) baadae AgaKhan Tambza. Utotoni kachezea Yanga kids na hao unao waona kwenye picha na wengine hawapo hapo akina Pondamali, Adolf richard, Sunday Manara nk.

    Upanuzi wa barabara ya morogoro road miaka ya mwishoni 1960 nyumba yao ilivunjwa na malipo yao marehemu mzee Dau ndio akajenga nyumba Magomeni Mapipa na ipo mpaka leo hii.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 23, 2012

    Picha ya kumbu kumbu nzuri, walichotibua ni kukosa nidhamu na mantiki yapicha.Yaani wamekaa kama wamelazimishwa vile, ni wachache tu ambao wamepozi mswano kwa mpiga picha.
    Dr Gangwe Bitozi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 23, 2012

    Hii ni kumbukumbu nzuri sana nawakumbuka hawa jamaa walikuwa na vipaji vya kweli japo hawakufika mbali sana kutokana na mfumo wa soka wakati huo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 23, 2012

    nyie mnao complain about pose za wapiga picha mlitaka wa act kama watoto waonyeshe vidole viwili.. peace..ama waonyeshe thumb up...nyie vipi hao ni watu wazima so wamepose kama watu wazima kueni na adabu kwa wanasoka wetu wakongwe

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 23, 2012

    Akutendeae Mema Kumshukuru ni Lazima
    Jaza ya mema ni mema
    Maovu kutoyatia

    Picha zooote za Dr na ma CEO wenzake yuko serious

    Akienda klabuni PAN hapo kariakoo inaonekana yuko more at home

    Inawezekana kabisa kuwa hao aliokaa nao hawamuudhi ma mastori ya Euro bailouts, sijui mambo ya Private Equity, sijui mambo ya ISSA...la hasha...hapo story ni za SOSPETER OCHIENG kwenye kombe la Gossage 1978. Nashangaa Captain Maliki siuji yuko wapi hapo haonekani

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 23, 2012

    Si kweli Dau si mtoto ma wagomeni mapipa. Dau kazaliwa pale Mwembe Togwa (siku hizi mmepabatiza jina mnapaita FIRE) huko magomeni mie naona alienda tuuu kutembea lakini kwao khaswa ni pale mwembe togwa sasa haya mambo ya kutaka kumlazimisha kuwa kwao ni magomeni nadhani ni kampeni tuu za jamaa wanaotaka wafadhiliwe na ile klabu yao lakini ukweli ni kuwa nasaba yake haswa ni KARIAKOO

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 23, 2012

    wengine mbona hatujawaona kama Ibrahim kiswabi,Jela mtagwa,Juma pondamali nk. swali la kizushi jengo la PAN AFRICAN LILIKAMILIKA?? Mdau Leicester.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 23, 2012

    Na wewe unayesema Dau katoka kariakoo hujui kitu, dau kazaliwa shinyanga kijij cha isebule na wakaamia kariakoo wakati yuko darasa la 6 na akahamia magomeni kagera wakati yupo form 3.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 23, 2012

    Hapo wamekosekana Juma Pondamali Mensah na Mohamed Rishard Adolf..big up wakongwe nyie ndo mlikuwa wachezaji wa ukweli..sio cku wachina kibao teehteeh.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 23, 2012

    " A picture is worth a thousand words",hongera kwa waliopozi maalum kwa hii picha.Over 84% of human communication is body language, kutomosa simu wakati wa picha ya pamoja siyo busara.
    Dr Gangwe Bitozi

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 23, 2012

    picha safi kabisa, hao woote my home boys

    mdau born town, kariakoo

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 25, 2012

    Tatizo kubwa ni katika kuwaenzi watu kama hawa!

    Huwezi amini unaweza kukuta hata kadi za Bima ya Afya hawana, hwajapatiwa pamoja na kutumika kwao ktk Soka nchini na kushiriki timu ya Taifa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...