ABE, bodi inayotoa kozi mbalimbali kutoka nchini Uingereza, yaandaa hafla fupi iliyowakutanisha wadau mbalimbali kujadili masuala ya elimu nchini Tanzania na matokeo yake katika ajira kwa vijana. Hafla hiyo ilishirikisha watu wenye taaluma mbalimbali kama vile watoa elimu, wanafunzi, makampuni ya ajira, maafisa wa rasilimali watu, wafanyakazi wa makampuni binafsi na serikalini, vyombo vya habari na wananchi wengine wanaoguswa na tatizo hilo. 

Katika hafla hiyo, jopo lililoteuliwa na waandaji liliongoza majadiliano yaliyowapa changamoto wadau kutafuta njia za kupunguza tatizo la idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza masomo kila mwaka ambao wanakosa nafasi za ajira. Majadiliano hayo yalitoa hamasa kwa wadau kubainisha ujuzi na vigezo vinavyohitajika zaidi na waajiri na namna ya kuwasaidia wahitimu kupata ujuzi huo. 

Akizungumza katika hafla hiyo, mwakilishi wa ABE nchini Tanzania, Bi Zaituni Ituja alisema, “Wote tunafahamu kuwa wahitimu wengi hawana ajira. Lakini pia tunasikia makampuni yanalalamika kuwa hawapati vijana wa kuwaajiri wenye vigezo. Je, tatizo ni kuwa makampuni hayajui pa kutafuta wafanyakazi au wanapata vijana wasiokidhi vigezo? Swali hili ndio chanzo kikubwa cha sisi kuandaa hafla hii na tunatarajia wadau wataona umuhimu wa kuendeleza mjadala huu na kufanyia kazi mapendekezo haya.” 

Mbali na majadiliano hayo, wageni walipata muda wa kufahamiana baina ya waalikwa kupitia zoezi la utambulisho lililoongozwa na mwendeshaji wa hafla hiyo. Waalikwa walipata fursa ya kubadilishana mawasiliano ya kibishara kwa lengo la kujenga mahusiano kama ilivyokuwa dhamira ya hafla hiyo katika kuwakutanisha wadau wa elimu na ajira Tanzania. 

ABE inafanya shughuli zake kwa zaidi ya miaka 40 katika nchi zaidi ya 100 duniani na imewekeza katika kuhakikisha inatoa kiwango cha elimu cha hali ya juu. Kozi zinazotolewa ni kozi za masomo ya biashara ambazo zinaweza kumsaidia mtu kupata shahada ya chuo au kumwezesha mtu kupanda cheo. ABE inatoa kozi za Business Management, Business Start-up and Entrepreneurship, Human Resource Management, Marketing Management na Travel, Tourism and Hospitality Management. 

Kozi hizi zinaweza kusomwa na watu ambao wako kwenye ajira na wanataka tu kukuza uwezo wao na kupanda cheo, au wanaotaka kutumia ABE kama njia ya kupata nafasi ya kujiunga na vyuo mbalimbali duniani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...