Na Lulu Mussa -Sumbawanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara yake siku ya leo Waziri Makamba ameshuhudia uharibifu mkubwa wa mazingira hususan pembezoni mwa ziwa Rukwa.

Waziri Makamba amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha Nankanga kwamba mwaka 2000 kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka 2016 chanzo hicho kimepungua hadi kufikia mita tatu. "Tafiti zinaonyesha kuwa kupungua kwa kina hicho pamoja na mambo mengine kunasababishwa na kilimo cha milimani na kandokando ya ziwa, na ulishaji wa mifugo katika Vyanzo vya maji" Makamba alibainisha

Katika ziara yake baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri Makamba ameazimia kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa mazingira na kanuni za matumizi ya maeno hayo zitaandaliwa ili kunusuru Ziwa Rukwa.

Pia, wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa kutenga pesa zitokanazo na tozo mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa alama maalum 'beacons' ili kuainisha eneo tengefu na kuagiza kuwa zoezi hili lifanyike haraka.

Aidha, Mhe. Makamba amesisitiza juu ya upandaji wa miti na ameonyesha masikitiko yake kwa Mkoa wa Rukwa kuwa na upungufu wa miti ya asili na ile ya kupanda kwa kiwango kikubwa. "nimetembea zaidi ya kilomita 200 sijaona miti iliyopandwa" Makamba aliongezea.

Wakazi wa Mkoa wa Rukwa wamefahamishwa na kusisitizwa kuwa kuanzia mwakani itakuwa lazima kwa wanafunzi wa Primary na Sekondari kuwasili na miti na kutakiwa kuitunza mpaka pale watakapomaliza shule. Waziri Makamba ameahidi kuleta wataalamu na kutoa orodha ya miche inayostawi katika kila kijiiji ili kurahisisha uoteshaji wa miti.

Katika hatua nyingine, Waziri Makamba amekutana na viongozi mbalimbali za dini na wazee wa Mkoa wa Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya Amani, na kuahidi kugharimia Mkutano wa kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo na kusisitiza agenda ya Mazingira iwepo.

Mkoani Rukwa Waziri Makamba ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo na Mkutano wa Hadhara katika Kijiji cha Nankanga ambapo wakazi wa maeneo hayo wamempongeza kwakua toka kijiji hicho kianzishwe mwaka 1974, Waziri Makamba ndio amekuwa mgeni wa kwanza Kitaifa kuwatembele.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Rukwa wakielekea kutembelea fukwe za ziwa Rukwa zilizoharibiwa vibaya 
 Sehemu ya wakazi wa Nankanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani) wakati wa Waziri akiwahimiza juu ya kutuza rasilimali za Mazingira. 
 Mifugo ikichungwa pembezoni mwa Ziwa Rukwa Waziri Makamba amegiza shughuli za aina hiyo kufanyika mita 200 kutoka kwenye chanzo cha maji
Sehemu ya Viongozi wa dini, siasa na wazee wa Mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani) alipokutana nao na kusisitiza amani na Hifadhi ya mazingira.



  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...