KATIKA moja ya mambo ambayo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa rais dokta John Magufuli inasisitiza kuyafanya ni kwa viongozi kushuka kwa wananchi kwa kuwatembelea ,kusikiliza kero zao na kuzitatua.

Ili kulitekeleza hilo mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu ameitenga siku ya alhamisi ya kila wiki kuhamishia ofisi yake kwenye tarafa maalum kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi kutoka kwa wahusika.

Alhamisi hii akiwa ameweka kambi tarafa ya Ihanja wilayani humo Mtaturu amemuagiza kaimu mkurugenzi wa wilaya hiyo Haika Massawe kumuelekeza mwanasheria wa halmashauri kutoa msaada wa kisheria kwa Fatma Mohammed ambaye anasumbuliwa kupata haki yake ya ardhi.

Mama huyo anafuatilia shamba la baba yake mzazi ambaye ni mzee na anaumwa lililovamiwa na mtu bila ya mafanikio pamoja na kwamba alishinda kesi katika baraza la kata na wilaya lakini alikatiwa rufaa mahakama ya rufaa ya Dodoma.

“Mkurugenzi fuatilia kwa mwanasheria ilia toe msaada wa kisheria,kesi hii imeelekezwa na jaji wa mahakama ya rufaa ya Dodoma kuwa kuna makosa yamefanyika kwenye baraza la kata huku,”alisema Mtaturu.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akimkabidhi mashuka Dk. Frank kwa ajili ya kituo cha afya cha Ihanja wakati akiwa katika ziara ya kukagua huduma zinazotolewa kituoni humo na kusikiliza kero za wananchi.
Dk. Frank wa kituo cha afya cha Ihanja akitoa maelezo mbele ya mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu na diwani wa kata ya Kituntu Said Tumbwi wakati walipofika kituoni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akikagua shamba la mtama la mwananchi wa kijiji cha Puma ikiwa ni muendelezo wa ziara yake aliyoifanya katika tarafa ya Ihanja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...