Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mbunge wa Jimbo la Ileje, Janet Mbene amewatoa hofu wakazi wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kutokuwepo kwa ujenzi wa barabara na kusema kuwa muda wowote kuanzia sasa Barabara ya Isongole Mpemba itaanza kujengwa.

Akizungumza na wakazi wa Ileje alipokuwa akijibu maswali kupitia mtandao wa kijamii wa Whats up, Mbene amesema kuwa Sasa hivi Evaluation ya tenda documents imemalizika.

“Wamemaliza kupitia makabrasha ya 'Tender' wanaendelea na majadiliano na Mkandarasi juu ya gharama na vipengele mbalimbali, na watamtangaza Mkandarasi muda si mrefu kabla ya Mwezi wa Sita kama nilivyoelezwa na meneja wa Tanroads mkoa wa Mbeya” amesema Janet Mbene.

Barabara hiyo ya Mpemba-Isongole ni moja ya barabara ambazo zipo katika ahadi ya Rais John Pombe magufuli hivyo muda si mrefu wakazi wa Wilaya ya Momba na Ileje wataunganishwa katika barabara hiyo.

Ujenzi wa barabara hiyo utaweza kuinua fursa za kiuchumi katika Wilaya ya Ileje hasa kufungua biashara za mipakani kati ya nchi ya Tanzania na Malawi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...