Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze

Waziri wa biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, amezitaka taasisi zinazohusika na uwekezaji kutokuwa na ukiritimba ili hali kufikia malengo ya serikali ya kukuza sekta ya viwanda.

Aidha ameeleza kwamba, wizara hiyo, imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yatawezesha kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.
Hayo aliyasema huko kitongoji cha Pingo Chalinze,Bagamoyo,wakati akiweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha Vigae cha Twyford Ceramics Ltd.

Mwijage alisema, uwekezaji huo unaendana na dhana ya Rais Dk John Magufuli wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda .Alisema kwa kuanzishwa viwanda vingi vya aina hiyo kutasaidia kuongeza pato la nchi na kuzalisha ajira kwa wingi.

“Zipo idara ambazo zinafanikisha uwekezaji ikiwemo brela, idara ya uhamiaji, kazi, mamlaka ya mapato TRA, wizara ya ardhi, shirika la viwango TBS, baraza la Mazingira NEMC ambazo zinapaswa kufanya kazi kwa wepesi ili kufanikisha uwekezaji,” alisema Mwijage.
Ramani ya kiwanda
Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Magid Mwanga ,wa pili kushoto mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo na Jack Feng mkurugenzi wa kiwanda, wa tatu kushoto ni waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage na Ridhiwan Kikwete na Cliford Tandari wakiweka udongo kwenye jiwe la msingi.(picha zote na Mwamvua Mwinyi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...