Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 25, 2017 amefanya ziara ya kutembelea Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam.

Ziara hiyo ilikuwa na dhamira ya kubaini na kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo hususani changamoto ya Upungufu wa Madarasa na Vyoo kwa ajili ya Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo.

Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya Kibamba, Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Mabibo, Mtendaji Kata ya Mabibo, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa, Uongozi wa vyama vya siasa, Kamati ya Shule, Walimu sambamba na Wazazi.

Katika ziara hiyo Mhe Makori amefikia uamuzi wa kuchangia Shilingi Milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule kutokana na ubovu wa vyoo vilivyopo huku akiwasihi wananchi kwa ujumla kujitokeza kuchangia ujenzi wa vyoo hivyo.

Aidha ameahidi kuanzisha Harambee mahususi kwa ajili ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa kwani yaliyopo ni Madarasa 22 Kati ya Madarasa 68 hivyo kuna upungufu wa madarasa 46.

Kwa upande wa Matundu ya vyoo alisema kuwa upungufu ni mkubwa kwani yanahitajika matundu 136 na matundu ya vyoo yaliyopo ni 26 pekee hivyo kuna upungufu wa matundu 110.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na walimu pamoja na wazazi katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 25, 2017
Wazazi na Walimu wa Shule ya Msingi Kawawa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisalimiana na Ally Khamisi Mvugalo mara baada ya kuwasili katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi. Leo Mei 25, 2017
Moja ya Majengo yaliyochakaa Shule ya Msingi Kawawa Iliyopo katika Kata ya Mabibo Manispaa ya Ubungo

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ujenzi wa Manispaa ya Ubungo unakamilika lini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...