Wadhamini wakuu wa Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, jana ilitoa zawadi zenye thamani ya shilingi 232,974,660 kwa washindi mbali mbali wa ligi.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi Mkuu wa biashara na Masoko wa kampuni hiyo,Hisham Hendi alisema Vodacom imeongeza kiasi cha fedha zaidi mwaka huu.

Mwaka jana tulitoa shilingi 219,502,500. Kwa ajili ya zawadi lakini mwaka huu fedha hizi zimeongezeka na kufikia shilingi 232,974,660,” alisema

Hendi alisema, Vodacom Tanzania inavutiwa na jinsi ambavyo umaarufu wa ligi unavyokuwa ukiongezeka siku hadi siku huku ukiwavutia na kuwaburudisha Watanzania walio wengi wanaoishi mijini na vijijini bila kujali kama timu za maeneo wanayoishi zinashiriki ligi hii.

“Pamoja na umaarufu wa ligi hii kuongezeka na mafanikio yanayozidi kupatikana, sisi kama wadhamini tunajua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali za kuboresha ligi yetu iwe na viwango vya hali ya juu na ili kuondokana na changamoto hizi unahitajika ushirikiano mkubwa baina ya wadau wote wa mchezo wa soka nchini japo mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja,” alieleza.

Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wadau wote kushiriki kubuni mikakati ya kuboresha ligi hii na ikiwezekana wajitokeze wafadhili wengine zaidi ili wachezaji wazidi kunufaika.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(kushoto) wakimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuchukua tuzo hiyo hapo jana wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella, akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 84/- Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa baada ya timu yao kuibika mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (kushoto) akimkabidhi tuzo ya heshima, Kitwana Manara wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) akimshuhudia Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi(kushoto)akimpongeza baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...