Wamiliki wa Showroom za kuuza Magari leo wamepelekwa Kigamboni kwenye eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya Kuuza Magari (Dar es Salaam Automobile Zone) kwaajili ya kukagua  eneo hilo na kuonyeshwa namna ya kumilikishwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amesema eneo hilo litamilikishwa kwa Wamiliki wa Showroom kwa Muda wa Miaka Mitatu ya Mwazo Bure kisha Baada hapo watawekewa utaratibu wa Malipo.

Amesema Wamiliki hao watatakiwa kutoa kiasi cha Shilingi 300,000 kama dhamana ya kuonyesha nia. Amesema kuwa ukubwa wa eneo lilitengwa kwaajili ya Showroom ni Square Meter 750,000 ambapo lipo eneo lingine la ziada lenye ukubwa wa kiasi cha Square Meter zaidi ya 300,000.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya Kigamboni Rahel Mhando amesema mradi huo ni fursa kubwa ya Maendeleo kwa Wilaya hiyo. Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kubuni Mpango huo ambao pia utafanya Wilaya ya Kigamboni kuwa kwenye mpangilio Mzuri.

Nae Salim Chicago ambae ni mmiliki wa Showroom amesema Mpango huo utawapa unafuu wa kupata huduma zote ikiwemo TRA, TPA,BIMA,SUMATRA,Kituo cha Polisi na huduma za Kibank ndani ya eneo moja. Aidha amesema Mpango huo utawarahisishia kupata Wateja wengi na wa uhakika kutoka ndani na Nje ya Nchi.
Hata hivyo amesema utaratibu huo utawawezesha kulipa kodi ya Serikali na kuwabana wale Wafanyabiashara wanaofanya biashara za magari kwenye maeneo bubu.

Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alitoa agizo la kuwataka wenye Showroom na Yard za kuuza Magari kuhakikisha wanahamia Kigamboni kwenye eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya Showroom kabla ya Mwezi January Mosi mwakani.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa (wakwanza kushoto) akizungumza na wamiliki wa Showroom za kuuza Magari katika eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya Kuuza Magari (Dar es Salaam Automobile Zone).
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa (katikati) akiwaonesha wamiliki wa showroom eneo lililotengwa kwaajili ya biashara ya magari Kigamboni jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...