THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.
TAARIFA KUTOKA JENZI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E”            Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463       Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                        DAR ES SALAAM, 20 Octoba, 2014
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.
          Aidha,  kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare za JWTZ.  Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare hizo sheria itachukua mkondo wake. 

  
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963


TAARIFA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MEJA JENERALI (MSTAAFU) ROLAND MAKUNDA
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
 
Simu ya Upepo   : “N G O M E”          Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463      Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                       DAR ES SALAAM, 20, October, 2014
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa ya ratiba ya kuaga mwili wa Meja Jenerali Roland Makunda (Mstaafu) aliyefariki tarehe  16 Octoba 2014 wakati akipata matibabu katika Hospitali Kuu ya Kijeshi Lugalo.
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dr Hussein Mwinyi  leo tarehe 20 Octoba 2014 mnamo saa nne kamili anatarajia kuongoza Makamanda, wapiganaji na watumishi wa umma katika kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Roland Makunda kwenye viwanja vya Hospitali ya Lugalo.
 
  
 
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963


UNESCO BADO KURIDHIA UJENZI BWAWA LA STIEGLER’S GORGE KUFUA UMEME

UNESCO-logo1
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati yake na mamlaka husika nchini Tanzania za kuwezeshwa kujengwa kwa bwawa la kufua umeme la Stiegler’s Gorge .

Ofisi za Shirika hilo zilizopo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki wametoa taarifa ya kukanusha maelezo yaliyoandikwa na gazeti la The Guardian (ref:http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=72984) kwamba yapo maafikiano kuhusu ujenzi wa bwawa hilo.

Eneo la Stiegler’s Gorge lipo katika hifadhi ya Selou ambayo ni sehemu ya urithi wa kimataifa ambapo ujenzi wa miundombinu yoyote yenye athari kubwa katika hifadhi hiyo lazima kuwepo na maridhiano kati yake na mamlaka husika.

Taarifa hiyo imesema taarifa zilizoandikwa na gazeti hilo Oktoba 8, mwaka huu limeshutua shirika hilo. Taarifa hizo zilizokuwa ukurasa wa mbele zilisema kwamba Tanzania itavuna zaidi nishati ya umeme kutokana na maafikiano yake na UNESCO juu ya ujenzi wa wa bwawa hilo.

Katika taarifa yake UNESCO imesema kwamba katika mkutano wa 36 wa kamati ya Urithi wa dunia (WHC) uliofanyika Saint-Petersburg mwaka 2012 na ule wa 37 uliofanyika Phnom Penh, mwaka 2013 na wa mwisho uliofanyika Doha mwaka huu ulieleza wazi mashaka yake juu ya athari ya ujenzi wa bwawa hilo katika hifadhi.

Katika mikutano yote hiyo ilikubalika kwamba mamlaka zinaozohusika nchini kutofanya shughuli zozote za maendeleo ndani na kwenye mipaka ya hifadhi bila kupata kibali cha WHC kwa mujibu wa kifungu 172 cha makubaliano.

Aidha kamati hiyo iliitaka mamlaka zinazohusika kutekeleza ushauri uliotolewa na kamati ya pamoja kati ya WHC na Muungano wa ushirikiano wa hifadhi ya asili (IUCN) wa kutengenezwa kwa mkakati kabambe wa menejimenti ya Ekolojia ya Selous. Aidha inatakiwa kutayarisha menejimenti hiyo kwa kuweka mipaka katika eneo la urithi wa dunia na kuonesha maeneo ambayo yanastahili kuingizwa katika hifadhi.

Pia kufafanua mradi wa Stiegler's Gorge, hatua iliyofikiwa hasa katika maamuzi na kuhakikisha kwamba ufahamu kuhusu athari, gharama, manufaa na namna inavyofaa au kutofaa na pia kuwa na mpango mbadala kama haikuwezekana. Mambo yote hayo yanatakiwa kuzingatia umuhimu wa eneo hilo kwa jamii ya dunia na hivyo kuangalia vigezo vyote vya maeneo ya urithi .

Katika maamuzi hayo pia Kamati ya Urithi ilifurahishwa na nia ya mamlaka husika za Tanzania kuendesha utafiti huo kwa mujibu wa makabaliano na vigezo stahiki ili kuelewa athari zake katika hifadhi hiyo ambayo ni urithi wa kimataifa, korido za mapito ya wanyama na nini kitatokea kwa korido la Selous-Niassa Corridor.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO, kamati hiyo ya Urithi wa Dunia (WHC) ilitarajia kupata taarifa za awali Februari Mosi mwakani. Aidha taarifa hiyo ilitakiwa kuwa na muhtasari wa hatua mbalimbali zinazchukuliwa na muda wake kuhusiana na hifadhi ya Selou kujiondoa katika urithi wa dunia ulio katika hatari ya kutoweka.

Imeelezwa kuwa taarifa hiyo ndiyo itakuwa msingi wa majadiliano katika mkutano ujao wa WHC wa 39 utakaofanyika Bonn Ujerumani. Aidha taarifa hiyo imesema kutokana na vitu vyote kutokuwa bado kufanyika msimamo wa UNESCO unabaki kama ulivyo, kwamba hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa na kinyume na hapo ni kukiuka makubaliano.


SIMBANET YAFANYA SIKU YA FAMILIA

 Kampuni ya SimbaNET (T) Linited ya jijini Dar es Salaam Jumamosi hii iliandaa bonanza la michezo lililowakutanisha pamoja wafanyakazi wa kampuni hiyo na familia zao. Siku hiyo ilikuwa ni ya kula kunywa na kuchezo michezo ya aina mbalimbali ikiwepo soka, kuvutana kamba, kuogelea, muziki na michezo mbalimbali ya watoto. Kampuni ya Seree ndio walikuwa waandaaji wa tafrija hiyo iliyofanyika kwa mafanikio makubwa katika ufukwe wa Hoteli ya Bahai Beach.
 
 wafanyakazi na familia zao wakichukua kifuangua kinywa mara baada ya kuwasili bahari Beach Hotel.HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


FACEBOOK KUTUMIKA KUFUNZA USALAMA BARABARANI

DSC_0135
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (wa pili kushoto) akifurahi jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. 

Kushoto ni Mratibu wa Mradi wa kuboresha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (wa pili kulia) nje ya ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili katika warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP). (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, amekubaliana na haja ya kuanzisha mafunzo katika vyombo vya habari vya kijamii kama facebook ili kutanua uwanja zaidi wa elimu ya usalama barabarani hasa kwa vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa ajali.

Aidha amesema Polisi wanafikiriia kuanzisha mfuko wa kielektroniki wa ulipaji wa faini kwa makosa ya barabarani ili kuongeza kasi ya udhibiti na kuondoa tuhuma za rushwa.

Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanahabari na watendaji kutoka redio za jamii nchini mjini Dodoma, katika warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP).

washa ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
DSC_0141
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph, akisalimiana na Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, mara baada ya kuwasili kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.


BI REHEMA AMEPOTEA KWA YEYOTE ATAKAYEMUONA ANAOMBWA KURIPOTI KITUO CHA POLISI KIGAMBONI U KILICHO KARIBU

Bi Rehema Salum Msambya pichani juu amepotea tokea tarehe 16/10/2014 maeneo ya Kigamboni - Kisota karibu na Shule ya Sekondari ya Abdu jumbe. 
Siku hiyo alikuwa amevaa Dela Na Skintirt ya Rangi ya Blue. Bi Rehema ana Matatizo ya Akili. Yeyote atakayemuona anaombwa kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Kigamboni au kilicho karibu  au Apige simu namba
0712 22 77 22
0753 63 49 67
0712 70 77 87
0713 23 52 94


KAMPUNI YA TWIGA CEMENT YATOA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI BORA WA MATOFALI

 Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Simon Delens, akizungumza wakati wa semina kuhusu utengenezaji wa bora wa matofali waliyowaandalia watengeneza matofali na wasambazaji wao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Undelezaji Biashara wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Danford Semwenda, akitoa mada wakati wa semina kuhusu utengenezaji wa bora wa matofali waliyowaandalia watengeneza matofali na wasambazaji wao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Afya, Usalama na ulinzi wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Alfred Anthony akizungumza wakati wa semina hiyo.
Meneja Usambazaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Tumaini Joseph akizungumza wakati wa semina hiyo waliyowaandalia watengeneza matofali na wasambazaji wao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Ofisa mahusiano na Huduma kwa Weteja wa Kampuni ya Twiga Cement (TPCC), Martha Haule (kushoto) akizungumza katika semina hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa washiriki wa semina kuhusu utengenezaji bora wa matofali, Mary Kimaro (kulia) akipokea cheti kutoka kwa  Meneja Uendelezaji wa Biashara wa Kampuni ya Twiga Cement (TPCC), Danford Semwenda mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo iliyoandaliwa na TPCC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja  Afya, Usalama na Ulinzi wa kampuni hiyo, Alfred Anthony.


ngoma azipendazo ankal

Nay wa mitego Ft. Diamond platnumz - Muziki gani


JK akiongea katika hafla ya tuzo za CNN MultiChoice za waandishi wa habari Afrika 2014


CHINA KUWEKEZA BAGAMOYO

Na John Gagarini, Bagamoyo
JIMBO la Jilin nchini China limekubali kuwekeza hapa nchini kwenye eneo la Uwekezaji la (EPZ) la Kamal lililopo Kijiji cha Kerege kwa Kikwete wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Uwekezaji huo utafanyika baada ya ujio wa baadhi ya viongozi wa Jimbo hilo kutembelea maeneo mbalimbali ya uwekezaji wilayani humo na kuonekana kuvutiwa na sehemu hiyo.

Akizungumza jana mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa akiongozana na mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na sekretarieti ya mkoa wa Pwani na kuvutiwa na eneo hilo la uwekezaji la EPZ, Naibu Gavana wa Jimbo hilo Zhoncheng Sui alisema ameridhika na eneo hilo.

Sui alisema kuwa kutokana na urafiki wa kihistoria uliyopo kati ya Tanzania na China toka enzi za viongozi wa mataifa hayo Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tse Sung kumekuwa na ushirikiano ambao ni wa damu hivyo lazima udumishwe kwa ushirikiano wa kimaendeleo.

“Tumeona mambo mengi ambayo tunaweza kushirikiana ambapo moja ni pale kwenye eneo la uwekezaji ambapo tutakuja kuwekeza hapo kwani kuna miuondombinu mizuri ya barabara, maji na umeme pia waiteni na wenzetu waliopo hapa Tanzania ili nao waje wajionee na kuangalia namna wanavyoweka kuwekeza kwenye mkoa huu wa Pwani,” alisema Sui.

Awali akimkaribisha naibu gavana wa Jimbo hilo la Jilin mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza alisema kuwa mkoa wa Pwani una mambo mengi ambayo wawekezaji wanaweza kuwekeza ikiwa ni pamoja na kwenye kilimo, uvuvi, utalii na mifugo.

“Fursa zipo nyingi ndani ya mkoa wetu na hata miundombinu ya barabara, anga, bandari, uememe na reli viko vizuri kwa ajili ya kufanikisha uwekezaji ambao una hitaji uwepo wa mawasiliano mazuri,” alisema Mahiza.

Ujumbe huo ulikuwa na ziara ya siku moja wilayani Bagamoyo kutembelea maeneo ya uwekezaji kwenye ujenzi wa soko la kimataifa la samaki, eneo itakapojengwa bandari na eneo la uwekezaji la Kamal.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mwantumu Mahiza (katikati),Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Ahmed Kipozi (mwenye shati la kitenge) na Naibu Gavana wa Jimbo la Jilin nchini China Zongcheng Sui (pili kulia) wakiangalia bomba la maji ambalo limepasuka na kumwaga maji wakati ujumbe wa jimbo la China ulipotembelea jana eneo la uwekezaji la Kamal Kerege wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akiongea na Naibu Gavana wa Jimbo la Jilin nchini China Zhongcheng Sui alipotembelea wilaya ya Bagamoyo kuangalia maeneo ya uwekezaji.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka jimbo la Jilin nchini China pamoja na watumishi wa wilaya ya Bagamoyo mara baada ya mkutano uliofanyika Oceanic Bay Hotel $ Resort mjini Bagamoyo.


Spika Makinda aendelea na ziara yake nchini Oman

Spika wa Bunge Mhe Anne Semamba Makinda akipata maelezo toka kwa Katibu wa Bunge la Oman,Ali Nasser Al Mahrouqi ya namna mfumo wa kisasa wa uendeshaji Bunge ulivyo katika Bunge la Oman. Bunge hilo limeanza mfumo wa kutotoa hotuba/nyaraka kwa makaratasi na sasa wanatoa kwa njia ya mtandao (e-parliament).Wa pili kulia Mhe Sheikh Khalid Hilal All Maawali akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Mhe Mussa Zungu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Mheshimiwa William Lukuvi akiongea na Spika wa Bunge la Oman Sheikh Khalid Al Maawali.Mhe William Lukuvi ambae pia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge ni miongoni mwa wabunge nane wanaoambatana na Mheshimiwa Spika katika ziara rasmi ya kibunge nchini Oman.
Mhe Spika Sheikh Khalid Al Maawali akifafanua jambo kwa Mheshimiwa Spika Makinda kuhusu ukumbi wa Bunge la Majlis A'Shura.
Mheshimiwa Spika Makinda akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Oman TV kuhusu ziara yake.
Mheshimiwa Spika akimkabidhi zawadi ya picha ya mlango wa Zanzibar Spika wa Bunge la juu la Oman Majlis Doula, Mheshimiwa Dr Yahya Al Mandhary.Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania Oman Mheshimiwa Ally Saleh.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akizungumza na Wabunge wenzake waliomo katika msafara. Picha zote na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA SHEREHE YA KUWEKWA WAKHFU ASKOFU MTEULE WA KANISA LA AFRICAN INLAND DAYOSISI YA MWANZA, MCHUNGAJI JOHN BUNANGO, JIJINI MWANZA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana nabaadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, Oktoba 19, 2014, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, iliyofanyika jijini humo leo mchana.
Maaskofu wakimwekea mikono ya Baraka Askofu mwenzao, Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, wakati akiwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, Oktoba 19, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristu, waliohudhuria katika Sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo Oktoba 19, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya kuwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Oktoba 19, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu na wanafamilia ya Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya sherehe za kuwekwa wakhfu zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, machana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu wakati akiondoka kwenye uwanja wa CCM Kirumba, baada ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, leo Oktoba 19, 2014. Picha na OMR.


MANGULA, NAPE WAONGOZA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE YA VIJANA WA CCM VYUO VIKUU , LEO

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akihutubia Jumuia ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu katika Kongamano la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, lililoandaliwa na Vijana wa CCM wa Vyuo Vikuu, kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, leo, Oktoba 19, 2014.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika Kongangamano hilo la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Nape amewataka wasomi kutofumbia macho matatizo ndani ya CCM, badala yake wakati wakisifu  mema wawe mstari wa mbele kuyafichua na kuyakemea mapungufu ili chama kiende na wakati
Washiriki wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kongamano


AFRIKA KUSINI WATWAA UBINGWA WA SAFARI POOL AFRIKA 2014

Rais wa Chama cha Pool Africa(AAPA), Saths Reddy(kulia) akimkabidhi Meneja wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya mchezo wa Pool, kitita cha Dolla 5000 sawa na pesa taslimu za kitanzania 8,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Pool Africa(AAPA), Saths Reddy(kulia) akimkabidhi Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa Pool kitita cha Dolla 2000 sawa na pesa taslimu za kitanzania 3,400,000/= mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Taifa wa mchezo wa Safari Pool Tanzania, wakishangila wakiwa na kitita cha Dolla 2000$ sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali za Silva mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles), Ishmael Mthethwa kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla 2,000 sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.


TAMASHA LA FIESTA LAFANA,DAVIDO,ALI KIBA,DIAMOND WAZUA GUMZO KWA MASHABIKI,T.I AWAKUNA WABONGO

Mmoja wa askari waliokuwa wamepangwa katika suala zima la kusimamia usalama ndani ya tamasha la Fiesta 2014 akihakikisha usalama wa kutosha unakuwepo katika eneo hilo,na watazamaji wanapata burudani iliyokusudiwa kutoka kwa wasanii mbalimbali waliotumbuiza usiku wa kuamkia leo katika tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Shaa na madansa wake wakilishambulia jukwaa. 
Pichani kulia ni Msanii kutoka nchini Nigeria ajulikanae kwa jina la Kisanii Davido sambamba na Diamond Platnum kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la fiesta 2014 usiku wa kuamkia leo.
Msanii kutoka THT,Barnaba akiimba wimbo wake wa Wahalade sambamba na madansa wake kwenye jukwaa la fiesta 2014,katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Sehemu ya  umati wa watu waliokuwa wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Ilikuwa ni shoo moja nzuri kutoka nyumba ya vipaji ya THT
Pichani msanii Linah (nyeupe) akiwa na skwadi lake mara baada kumaliza kulishambulia jukwaa kwa pamoja.
Anaitwa Ally kiba ambaye inaelezwa kutoka kwa mashabiki  kuwa alifanyo shoo nzuri na iliyowavutia,na kuthibitisha uwezo wake kuwa ni kweli amerejea kwenye kiti chake cha usanii.
  Msanii kutoka nchini Marekani Clifford Haris a.k.a T.I akilishambulia jukwaa la Fiesta vilivyo
 Msanii kutoka nchini Marekani T.I akiwaimbisha mashabiki wake


BALOZI IDDI AKUTANA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Bwana Egon Kochanke ofisini kwake vuga Mjini Zanzibar.
Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Bwana Egon Kochanke akibadilisha mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika jitihada za kuimarisha ushirikiano kati ya Ujerumani na Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.