Katibu wa bakwata Mkoa wa Arusha Bw. Abdulkarimu Jonjo akiugulia maumivu katika wodi ya majeruhi ,katika hospitali ya mkoa mount Meru baada ya kulipuliwa na bomu la kutupwa na mkono akiwa amelala usingizini nyumbani kwake na watu wasiofahamika majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo. Picha na Josefu Ngilisho.

KATIBU mkuu wa Bakwata mkoani Arusha,Abdulkarim Jonjo (52) mkazi wa Esso jijini Arusha,amenusulika kufa baada ya kujeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospital ya Mkoa Mount Meru baada ya watu wasiojulikana kumlipua kwa bomu la kurushwa kwa mkono akiwa amelala usingizini nyumbani kwake. 

Akiongea kwa taabu katika wodi ya majeruhi hospitalini hapo,Jonjo alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 6.30 usiku akiwa amelala baada ya kuona mwanga wa cheche dirishani kwake na kufuatiwa na kishindo cha mlipuko. 

Alisema kuwa hali hiyo ilimlazimu kuinuka kitandani kuangalia tukio la mwanga huo wa cheche,lakini kabla ya kuufikia alisikia kishindo cha mlipuko mkubwa kilichosababisha kujeruhiwa vibaya baada ya kurushwa umbali ndani ya chumba chake. 

 ‘’unajua jana nilichelewa kulala kutokana na umeme kukatika nilikaa sebuleni hadi saa 5 kasoro dakika 20 nikaenda kulala ,lakini ilipofika majira ya saa 6 kasorobo niliamka kuchaji simu yangu baada ya kuona umeme umerudi na kwenda kulala ,ila ilipofika saa 6.30 ndipo nilisikia cheche dirishani na kufuatiwa na mlipuko’’alisema Jonjo. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus SABAS ameapa kuwasaka waliohusika na tukio hilo linalofananishwa na ugaidi na kuwafikisha mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. haya sasa mbona wenyewe kwa wenyewe?? me nasema tunaelekea kama nigeria na kundi la boko haram hapo watasema ni malipizi ya wakristo kumbe hakuna lolote ni watu tu hao wanatakapa kuupaka matope usilamu na pia wanaotaka kufanya nchi isitawalike na wanataka kuleta vita vya wenyewe kwa wenyewe hizi ni kazi za shetani kabisaa we umewahi kuona wapi mtoto anapata nguvu ya kukojolea kitabu kitakatifu kwani hakufundishwa kwao kwamba anatakiwa akiheshimu na kukitunza, tusipokua macho tutauana wenyewe kwa wenyewe

    ReplyDelete
  2. Harakati za Kidini zimefikia pagumu nchini Tanzania!

    Hivi wandugu pana Kitabu chochote Kitukufu cha Kiimani kinachosisitiza kuwa ukuaji wa Kiimani wa kundi moja ni kuwafanyia Ubaya dhidi ya wengine?

    Tutafakari kwanza maana ya Dini ni kuwa na Ustaarabu wa hali ya juu na kiwango cha juu cha Ubinaadamu na huruma dhidi ya wengine!

    Hivi kweli Ubaya unaenda sambamba na Uumini wa Dini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...