Hatimaye kundi la BONGO DANSI limetimiza mwaka mmoja kamili tokea kuanzishwa kwake na kufanya sherehe kubwa za maadhimisho katika ukumbi wa Vijana Social Hall.

BONGO DANSI ni kundi linalopatikana kwenye mtandao wa Facebook (kama Facebook Group) lenye lengo ya kujadili  na kuinua muziki wa dansi wa Tanzania sambamba na kuwaunganisha wadau mbalimbali wa tasnia ya muziki wa dansi Tanzania wakiwemo washabiki, wanamuziki, waandishi wa habari, mameneja na wamiliki wa bendi. Mpaka sasa kundi lina wanachama zaidi ya 3000.

Kundi la BONGO DANSI lilianzishwa rasmi tarehe 14-Aug-2013 na mwaka huu tarehe 14-Aug-2014 lilitimiza mwaka mmoja kamili wa uwepo wake. Kundi lilifanya sherehe ya maadhimisho ya mwaka mmoja Jumapili ya tarehe 17-Aug-2014 katika ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni ambapo lilijumuika kwenye show ya bendi nguli ya Vijana Jazz Band “Pambamoto, Saga Rhumba”.

Katika tukio hilo mwanamuziki wa zamani wa Vijana Jazz, mpiga solo Miraj Shakashia “Shakazulu” (ambaye pia ni mwana BONGO DANSI) alikuwepo kusalimia kisanii ambapo alishirika kupiga nyimbo mbili za “Ogopa Tapeli” na ”Penzi Haligawanyiki Part I”. Mwanamuziki mwingine aliyekuja kusalimia kisanii ni Alpha Kabeza wa Malaika Music Band aliyeimba wimbo wa “Acha Tamaa”, wimbo alioutunga alipokuwa FM Acadsemia “Wazee wa Ngwasuma”.

Akiongea kwa niaba ya BONGO DANSI, mratibu wa kundi, William Kaijage alilipongeza kundi la Vijana Jazz kwa kuwa bendi pekee nchini iliyobaki inayomilikiwa kitaasisi na pia kuwa moja ya bendi kongwe zaidi zilizobakia nchini na Afrika baada ya kuanzishwa mwaka 1971 miaka 43 iliyopita.

Mwana BONGO DANSI mwingine, Rajab Zomboko akitoa hotuba, aliwaasa wanamuziki wa muziki wa dansi kutumia mitandao ya jamii (social media) kujitangaza kama wanavyofanya wanamuziki wa bongo flava kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia.

Mtandao wa BONGO DANSI unapatika kwenye link hii https://www.facebook.com/groups/bongodansi/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...