Mwenyekiti wa Kikundi cha Tujiajiri Group cha Tarafa ya Nyasa wilaya ya Nzega Bw.Fanuel Kifunyu(waKwanza kulia)akiongea na kuonyesha ujumbe kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuhusu Bidhaa mbalimbali wanazotengeneza zikiwamo Sabuni,matofali ya kufungamana,na karanga baada ya kupata mafunzo ya mfuko wa Maendeleo ya Vijana,Stadi za Maisha,Ujasiriamali na Uongozi Bora.Wengine pichani ni Afisa Vijana Laurean Masele(wa pili kutoka kulia),Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji(katikati) na Afisa Vijana Amina Sanga(Mwenye kiremba cha Njano.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji Bi.Esther Riwa akimwuliza maswali Mwanakikundi cha Ushonaji na utengenezaji wa Viatu Bw.Chepe changamoto gani wanazokutana nazo katika ufanyaji wao wa kazi za ushonaji uku mwanakikundi uyo akibainisha kutopatikana wa mashine za kutengenezea viatu ivyo mpaka nchi jirani ya kenya.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji Bi.Esther Riwa(wa Kwanza kushoto) akipita katika shamba la nyanya la kikundi cha Nserema kinacholima Nyanya,Matikiti,na Kabeji kutoka  kijiji cha Iyombo Tarafa ya Nyasa.kikundi icho kinategemea kuomba mkopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kuboresha kilimo chao kwa kununua pembejeo za kilimo,kununua mbegu bora na madawa ya kuulia wadudu.katikati mwenye shatu jekundu ni Mwenyekiti wa kikundi icho Bw. Stephen Ndikamara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...