JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
Hivi karibuni zimeibuka taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya
kijamii zikimnukuu Waziri wa Nishati na Madini, George B. Simbachawene akisema kuwa mitambo yote ya uzalishaji umeme
nchini inamilikiwa na Kampuni binafsi.
Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa taarifa hizi ni za uongo kwani
Waziri Simbachawene hajawahi kutoa tamko la kuwa mitambo ya kuzalisha Umeme
yote nchini ni ya kampuni binafsi bali alichosema ni kuwa, baadhi ya mitambo ni ya kampuni binafsi
na mingine inamilikiwa na Serikali.
Mitambo inayomilikiwa na Serikali ni:-
1 Kinyerezi
I (Gesi) yenye uwezo wa MW 150 ambapo MW 35 zimewashwa leo 12 Oktoba
2015;
2 Ubungo
I (Gesi) yenye uwezo wa MW 102 ambayo kwa sasa inazalisha MW 85;
3 Ubungo
II (Gesi) yenye uwezo wa MW 105 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;
4 Tegeta
(Gesi) yenye uwezo wa MW 42 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;
5 Nyakato
(Mafuta) yenye uwezo wa MW 60 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;
6 Kidatu
(Maji) yenye uwezo wa MW 204 ambayo kwa sasa inazalisha MW 27;
7 Kihansi
(Maji) yenye uwezo wa MW 180 ambayo kwa sasa inazalisha MW 45;
8 Pangani
(Maji) yenye uwezo wa MW 68 ambayo kwa sasa inazalisha MW 17;
9 Nyumba
ya Mungu (Maji) yenye uwezo wa MW 8 ambayo kwa sasa inazalisha MW 5;
10 Hale
(Maji) yenye uwezi wa MW 21 ambayo kwa sasa inazalisha MW 4; na
11Mtera (Maji)
yenye uwezo wa MW 80 ambapo mitambo yake imezimwa (MW-0);
Kwa hiyo, Jumla ya kiasi cha umeme
kinachopatikana katika mitambo hiyo kwa sasa ni Megawati 337 kati ya Megawati 870 zinazotakiwa kuzalishwa.
Mitambo inayomilikiwa na watu binafsi ni:-
1 IPTL
(Mafuta) yenye uwezo wa MW100 ambayo kwa sasa inazalisha MW 80;
2 Aggreko
(Mafuta) yenye uwezo wa MW 70 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;
3 SONGAS(Gesi)
yenye uwezo wa MW180 ambayo kwa sasa inazalisha MW 158; na
4 Symbion
(Gesi) yenye uwezo wa MW 112 ambayo kwa sasa inazalisha MW 74.
Hivyo mitambo hii ya watu binafsi inazalisha umeme wa kiasi cha Megawati
382 kati ya Megawati 462 zinazohitajika.
Ieleweke kuwa Serikali inajitahidi kuiwasha mitambo hiyo yote inayomilikiwa
na Serikali na Binafsi ili izibe pengo la umeme wa maji ambao umepungua kutoka
MW 561 hadi MW 88. Ili nchi isiwe na mgawo
wa umeme zinahitajika MW 1332 ambapo kwa sasa kiasi cha umeme kinachopatikana
ni Megawati 719.
Awali tulikuwa na upungufu wa megawati takribani 450 lakini tumefanya
juhudi za kuwasha mitambo mbali mbali tangu wiki iliyopita na sasa upungufu
uliobaki ni kati ya MW 200 na 250.
Serikali kupitia TANESCO inatoa rai kwa Watanzania kuendelea kuvumilia
kipindi hiki cha mpito kwani inajitahidi kwa hali na mali kuwasha mitambo
iliyobaki ya gesi ya Kinyerezi yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha
megawati 150 hivyo hadi ifikapo tarehe 20 Oktoba, 2015 hali ya upatikanaji wa
umeme itaanza kutengemaa.
Asanteni na poleni kwa usumbufu unaojitokeza.
Imetolewa
na;
WIZARA YA
NISHATI NA MADINI
Hivi kwanini kila siku mnakanusha na hamuwachukulii hatua hao wapotoshaji? Sheria zipo kwanini hamzifuati?
ReplyDeleteAsante kwa taarifa,tutawavumilia lakini mjitahidi bwana umeme unatuhangaisha sana huku mitaani.SIku ya Uchaguzi chondechinde hakikisheni umeme upo 24 hrs
ReplyDelete