Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Umoja wa Mataifa, Chitralekha Massey akiwapiga msasa baadhi ya waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.
Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Salma Ally Hassan (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR) wakati wa warsha ya siku moja 29 Aprili 2016 Mkoani Morogoro.
Na Benedict Liwenga.

Asasi za Kiraia pamoja na Taasisi za kutetea haki za binadamu nchini zimewaasa Waandishi wa Habari nchini kujikita katika kuhabarisha umma kuhusiana na masuala ya haki za binadamu ikiwemo mauaji ya watu wenye ualbino, mauaji ya vikongwe, ukatili dhidi ya watoto, pamoja na adhabu ya vifo.

Rai hiyo imetolewa leo na Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Salma Ally Hassan wakati wa Warsha ya siku moja iliyofanyika mkoani Morogoro yenye lengo la kuwajengea uelewa Wanahabri kuhusu Mpango wa Kimataifa wa kujitathmini juu ya Masuala ya Haki za Binadamu (UPR).

Bi. Salma ameeleza kuwa kutokana na tathmini ya masuala ya haki za binadamu nchini, vyombo vya habari havinabudi kuwa na uelewa mkubwa kuhusu umuhimu wa kuziongelea haki za binadamu kwani jamii imekuwa haizitambui baadhi ya haki hizo na kumekuwepo na kukithiri kwa vitendo vya uvunjifu wa amani yakiwemo matukio ya mauaji ya watu wenye ualbino, vikongwe pamoja na ukatili kwa watoto.

Ameongeza kuwa, baadhi ya watu nchini wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi kwa kuua watu ambapo watu wenye kuyasemea hayo ni Vyombo vya Habari lengo likiwa ni kukemea kuendelea kwa vitendo hivyo.“Uvunjaji wa haki za binadamu unafanywa na watu katika jamii, kwa mfano, mauaji ya Watu wenye Ualbino, mauaji ya vikongwe, pale sio Serikali inakua imevunja haki za binadamu, bali ni watu katika jamii”, alisema Bi. Salma.

Kwa upande wake Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bi. Chitralekha Massey ameeleza kuwa, ni vema Tanzania ikakubalina na mapendekezo yanayohusiana na masuala ya haki za binadamu yanayoendana na Dunia kwa ajili ya ulinzi wa haki hizo.

“Sisi kama Umoja wa Mataifa tunapenda kuona Tanzania inafanya uamuzi utakaosaidia kuboreshwa kwa haki za binadamu nchini kwani ni wakati sasa wa jamii kusema kwa uwazi kuwa mapendekezo hayo yatakuwa yenye manufaa kwao”, alisema Massey.Aidha, katika warsha hiyo, vyombo vya habari, jamii pamoja na Serikali wanajukumu la kulinda haki za binadamu na kuendelea kukemea matukio yanayovunja amani katika jamii.


Tarehe 9 Mei, 2016 Tanzania inatarajiwa kufanyiwa tathmini ya pili juu ya hali ya haki za binadamu nchini na Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa ambapo tayari Asasi za Kiraia na Watetezi wa haki za binadamu wamekwisha wasilisha mapendekezo yao kwa Wawakilishi wa nchi wanachama wa umoja huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2016

    Kiitikadi, ubepari (capitalism unatilia mkazo haki za binadamu kujikita katika ubinafsi zaidi ya umma; ujamaa (commonality) umma ni zaidi ya ubinafsi.

    Na mzozo huo hautaisha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...