THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TAARIFA YA PROF ABDULKARIM MRUMA,MWENYEKITI WA KAMATI MAALUM YA KWANZA YA UCHUNGUZI


MKUU WA WILAYA YA UBUNGO MHE KISARE ACHANGIA MILIONI MOJA UJENZI WA VYOO SHULE YA MSINGI KAWAWA


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 25, 2017 amefanya ziara ya kutembelea Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam.

Ziara hiyo ilikuwa na dhamira ya kubaini na kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo hususani changamoto ya Upungufu wa Madarasa na Vyoo kwa ajili ya Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo.

Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya Kibamba, Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Mabibo, Mtendaji Kata ya Mabibo, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa, Uongozi wa vyama vya siasa, Kamati ya Shule, Walimu sambamba na Wazazi.

Katika ziara hiyo Mhe Makori amefikia uamuzi wa kuchangia Shilingi Milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule kutokana na ubovu wa vyoo vilivyopo huku akiwasihi wananchi kwa ujumla kujitokeza kuchangia ujenzi wa vyoo hivyo.

Aidha ameahidi kuanzisha Harambee mahususi kwa ajili ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa kwani yaliyopo ni Madarasa 22 Kati ya Madarasa 68 hivyo kuna upungufu wa madarasa 46.

Kwa upande wa Matundu ya vyoo alisema kuwa upungufu ni mkubwa kwani yanahitajika matundu 136 na matundu ya vyoo yaliyopo ni 26 pekee hivyo kuna upungufu wa matundu 110.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na walimu pamoja na wazazi katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 25, 2017
Wazazi na Walimu wa Shule ya Msingi Kawawa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisalimiana na Ally Khamisi Mvugalo mara baada ya kuwasili katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi. Leo Mei 25, 2017
Moja ya Majengo yaliyochakaa Shule ya Msingi Kawawa Iliyopo katika Kata ya Mabibo Manispaa ya Ubungo

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


CCM YAKEMEA VIKALI MAUAJI KIBITI,YAVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUCHUKUA HATUA


RAIS MSTAAFU MWINYI AONGOZA MAZISHI YA KITWANA KONDO

Na. Eliphace Marwa - Maelezo.

RAIS Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika maziko ya mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Kitwana Kondo.

Mbali na Mwinyi wengine waliohudhuria maziko hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Tambaza ni Makamu wa Rais Mstaafu, Mohammed Gharib Bilal, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Salim Ahmed Salim na Edward Lowassa, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wengine.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Mzee Mwinyi alisema, marehemu Kondo alikuwa  ni mtu ambaye alijitoa katika kulitumikia taifa kwa moyo wake, hivyo mchango wake ni mkubwa katika kulitumikia taifa na hasa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam.

"Alikuwa ni rafiki yangu ambaye tumefahamiana kwa muda mrefu sana, tumepoteza mtu muhimu sana, lakini kazi ya Mungu haina makosa, tumuombee kwa Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi," alisema Mzee Mwinyi

Kwa upande wake, Kinana alisema, taifa na hasa wakazi wa Dar es Salaan wamepata pigo kubwa kwa kumpoteza mzee huyo ambaye bado busara zake zilikuwa zikihitajika.

"Alikuwa ni kiongozi wa jamii,alikuwa ni mwalimu wa watu wengi katika manbi mbalimbali, ni msiba mkubwa lakini nj kazi ya Mungu, tuendelee kumuombea apumzike kwa amani," alisema Kinana.

Naye, Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa alisema, kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Mzee Kondo ni vema uongoziu wa jiji kuangalia namna ambavyo barabara moja ya jiji hilo likapewa jina la KK ikiwa ni kuheshimu na kutambua mchango wake.

"Namuomba Mstahiki Meya, barabara moja uiite KK, itakuwa ni heshima kumuenzi Mzee Kitwana Kondo kwa kazi kubwa aliyofanya wakati wa uhai wake," alisema Lowassa.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) , Profesa Ibrahim Lipumba alisema, mchango wa Mzee katika taifa ni mkubwa lakini kwa bahati mbaya ni kama jmeshindwa kutambuliwa.

"Ni mtu ambaye bahati mbaya sana historia ya nchi yetu haitambui mchango wake katika kuleta uhuru wa nchii na kudumisha uhuru wa nchii," alisema Profesa Lipumba.

Akieleza chanzo cha kifo cha baba yake, mtoto wa kwanza wa marehemu Mzee Kondo, Stara Kondo alisema, Baba yake alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal Mei 18 kutokana na kuugua muda mrefu lakini alifariki juzi.

“Alikuwa anaumwa muda mrefu lakini hadi anafariki madaktari walisema alipata stroke (Kiharusi) na shinikizo la damu, tutamkumbuka kwa mambo mengi kwa sababu ni baba lakini alikuwa ni kichwa cha familia,” alisema Stara 
 Mwili wa aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo ukiwa ukiwa umeingizwa kwenye kaburi tayari kwa ajili ya maziko katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Dkt. Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Ghalib Bilal akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
 Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombare Mwilu akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Jaji Mstaafu Mark Bomani akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wananchi walioshiriki mazishi ya aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Mzee Kitwana Kondo wakiweka udongo wakati wa mazishi mapema leo jioni jijini Dar es Salaam.

Picha Emmauel Massaka,Globu ya jamii


BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA UBUNGO LAAGIZA IDARA YA MIPANGOMIJI KUFUATILIA NA KUTWAA MAENEO YA UMMA

Na Mathias Canal, Dar es salaam.

Baraza la Madiwani Manispaa ya Ubungo kwa kauli moja limeridhia na kuagiza Idara ya Mipangomiji na Mazingira kufuatilia na kutwaa maeneo kwa ajili ya matumizi ya Umma hususani maeneo ya Shule.

Aidha Baraza la madiwani limeagiza Idara hiyo ya Mipango Miji kutembelea na kupima eneo la shule ya Sekondari Matosa iliyopo Kata ya Goba ambalo eneo lake limesalia ekari 31 kati ya 22 huku eneo jingine likitumiwa na wananchi kinyume na utaratibu.

Pia imebainika kuwa hali ya ukusanyaji mapato inaendelea kukua kutokana na juhudi na utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato tangu kuanza kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo baada ya mgawanyo wa Halmashauri hiyo kutoka Manispaa Mama ya kinondoni.

Akijibu swali lililoulizwa kuhusu ubovu wa mashine za kukusanyia mapato POS Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa hajawahi kupokea malalamiko juu ya mashine hizo na kubainisha kuwa Manispaa imepata mtaalamu anayeshughulikia mashine hizo ambapo atatoa taarifa juu ya kiasi kilichokusanywa tangu kuanza kutumika kwa mashine hizo za POS.

Akiongelea kuhusu semina kwa madiwani MD Kayombo alikiri kuwa kuna umuhimu wa madiwani kupata semina hususani kwenye eneo la kanuni na sheria mbalimbali na pia katika sheria za manunuzi hivyo ameahidi kuandaa semina hiyo ili waweze kuelimika zaidi.

MD Kayombo akizungumzia suala la maendeleo ya jumla katika kuboresha miundo mbinu katika shule za Manispaa ya Ubungo alisema kuwa zitakuwa zikifanyika hatua kwa hatua katika kuhakikisha miundo mbinu inaboreshwa huku akibainisha kuwa katika kuinua elimu katika Shule za Manispaa ya Ubungo ujenzi wa Madarasa, Vyoo sambamba na Ukuta vitaanza kujengwa hivi karibuni katika shule ya Msingi Ubungo Plaza.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakiwa kwenye Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Waheshimiwa Madiwani wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakisoma muongozo wa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam


SHEIKH SHARIF MAJINI KUFANYA KONGAMANO MKOANI ARUSHA JUMAPILI HII.

Sheikh Shariff Majini kutoka jijini Dar es salaam ambaye kwa sasa yupo ziarani katika baadhi ya mikoa Tanzania Bara, Jumapili tarehe 28-05-2017 atafanya kongamano kubwa kwa ajili ya akina Mama wa Jijini Arusha katika ukumbi wa CCM Mkoa kuanzia saa mbili asubuhi.
Matayarisho yote yamekwisha malizika na Sheikh ameshawasili Jijini Arusha tayari kabisa kwa ajili ya kuendesha kongamano hilo.

Pamoja na kongamano hilo Sheikh atafanya visomo kwa ajili ya kuwaombea watoto wanafunzi wa Shule ya Lucky Viscent ya Arusha waliofariki katika ajali ya gari. Pamoja na watoto watatu walionusurika wanaopata matibabu Marekani ili wapate nafuu haraka waweze kurejea kwenye masomo yao.


MWAZISHI YA MZEE KITWANA KONDO YAFANYIKA JIONI YA LEO MAKABURI YA TAMBAZA JIJINI DAR

Baadhi ya Ndugu Jamaa na Marafiki wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Kigamboni na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mzee Kitwana Kondo wakielekea kwenye maziko yake,leo Alhamisi baada ya swala alasiri katika makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Mazishi ya aliyekuwa Meya wa Dar es salaam Mzee Kitwana Kondo jioni hii makaburi ya Tambaza jijini Dar
Mwili wa Marehemu Mzee Kitwana Kondo ukiingizwa msikitini kwa ajili ya kuswaliwa tayari kwa mazishi jioni ya leo ,katika Makaburi ya tambaza,jijini Dar.
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa Makaburi wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu kwa ajili ya Maziko katika Makaburi ya Tambaza,jijini Dar 


Licha ya kukiri shtaka kesi ya Ndama kusikilizwa kama kawaida.

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Kesi dhidi ya mfanyabiashara, Ndama Shabani Hussein maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto ya Ng'ombe imeamliwa kuendelea kusikilizwa baada ya mshtakiwa huyo kukana baadhi ya maelezo ya awali (PH), licha ya mwanzoni mwa wiki hii kukubali shtaka la utakatishaji wa fedha kiasi cha USD 540,000.

Mapema wiki hii, Ndama alikiri kutenda kosa hilo ambalo ni kosa la sita kati ya anayoshtakiwa nayo, na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikapanga leo iwe siku ya kusomewa maelezo ya awali (PH), kabla ya kumsomea hukumu yake.

Hata hivyo, wakati akisomwa Maelezo hayo na wakili wa serikali Christopher Msigwa Ndama alikana baadhi ya tuhuma na kukiri chache kitendo kilichofanya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Victoria Nongwa kuamuru kesi hiyo iendelee kama kawaida kwani tuhuma alizokataa mshtakiwa ndizo zinajenga msingi wa kesi.

Ndama anayetetewa na Wakili Jeremiah Mtobesya alikiri baadhi ya maelezo ya awali aliyosomewa na wakili wa Serikali Msigwa ikiwamo nyaraka zilizotumika kufungua akaunti iliyotumika kuingizwa hizo fedha, hundi zilizotumika kutolea hizo fedha, maelezo ya benki ‘bank statement’ na Swift massage.

Hata hivyo alikana baadhi ya maelezo ambayo ni sehemu ya kuunda shtaka hilo, na kusema kuwa hawajui wakurugenzi wa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited wanaotambulika Brela, Bushoboka Mutamura na Mujibu Hamis Taratibu.

Aidha alikanusha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited haikuwahi kuingia mkataba na Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited  na kwamba hakuwahi kuwagaia wabia wenzake fedha hizo taslimu kwa lengo la kuficha chanzo chake.

Baada ya mshtakiwa kukana baadhi ya PH Msigwa alidai mahakamani hapo kuwa kwa kuwa mshtakiwa alikuwa amekiri kosa ni rahisi kuthibitisha yaliyofanyika na kwamba kwa kadiri maelezo ya awali yalivyosomwa na majibu ya mshtakiwa basi ni jukumu la mahakama kuangalia kama maelezo aliyokubali yanakidhi kumtia hatiani ama kesi ianze kusikilizwa.

“Ili haki ionekane imetendeka na kwa vile mshtakiwa anakubali baadhi ya maelezo na mengine ameyakataa mahakama inaona ni vema kesi ianze kusikilizwa ili kila upande upate haki yake kwani mshtakiwa alitakiwa akubali shtaka hili bila ya kupinga lakini kwa kuwa amekana baadhi ya tuhuma ni wazi kuwa amekana shtaka”, amesema Hakimu Nongwa.

Baada ya kutolewa kwa amri hiyo, Msigwa ameiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi itatajwa tena Juni 6, mwaka huu.

Mei 16, 2017, Ndama alikubali shtaka la sita la kutakatisha fedha ambapo anadaiwa kuwa kati ya Februari 26 na Machi 2014, Dar es Salaam, akiwa mwenyekiti na mtia saini pekee wa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Limited na akaunti ya benki ya kampuni hiyo iliyoko kwenye  benki ya Stanbic alijihusisha moja kwa moja kwenye uhamishaji wa dola za Marekani 540,000 na kuzitoa huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la uhalifu la kujiapatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mashtaka mengine anayokabiliwa nayo ni kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.


PROF NDALICHAKO AWATUNUKU WAHITIMU WA MAFUNZO YA WAKATI UJAO YALIYOENDESHWA NA ATE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako amewataka wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao kujiendeleza zaidi ili kuweza kutimiza ndoto zao pamoja na kuwapongeza Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa juhudi kubwa wanazozifanya.

Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO) yaliweza kuhitimishwa leo kwa wahitimu 33 kutunukiwa vyeti na Waziri Prof Ndalichako.

Akizungumza kabla ya utoaji wa vyeti kwa wahitimu Prof Ndalichako alisema kuwa ana imani kubwa kuwa mafunzo waliyoyapata kutoka kwa wakufunzi wao watayatumia vizuri zaidi ni kutaka kuwaona wakiwa wamefika mbali zaidi.

"Programu hii kwangu ni fursa kwenu na mafunzo haya mkiyatumia vizuri yatawasaidia kuendesha maisha katika nyanja mbalimbali kazini, nyumbani, kwenye jamii na kwa kizazi chetu Kijacho," amesema Prof Ndalichako.

Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kutoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO) na kuwapongeza kwa juhudi kubwa wanazozitumia katika kuwainua wanawake kimaendeleo.

Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako akitunuku vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO), kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Waajiri (ATE) Almas Maige,  Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani kwa Nchi za Afrika Mashariki Mary Kawar.

  Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na wahitimu wakati wa mahafali ya mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO).
 Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani kwa Nchi za Afrika Mashariki Mary Kawar akizungumza na wahitimu kabla ya kupatiwa vyeti hivyo kwa wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO).
 Wakurugnezi kutoka mashirika na kampuni mbalimbali wakitoa ushuhuda wa  namna walivyoanza mpaka walipo sasa, anayezungumza wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya Barclays Abdi Mohamed.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 34, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 25, 2017.


 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
 Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji  Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
 Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Abdallah Bulembo akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Mhe. Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Mbunge wa Arusha Mjini  Mhe. Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.  

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


MHE. ANTHONY MAVUNDE ALIVYOELEZEA JINSI SERIKALI INAVYOWAWEZESHA WANANCHI KUKOPESHEKA KATIKA TAASISI ZA KIFEDHA


YANGA ILIVYOLETA SHANGWE BUNGENI LEO MAY 25,2017


Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2016/17 Yanga wametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania  Mkoani Dodoma ikiwa ni katika ziara yao ya kuelekea Mkoani Arusha kwa ajili ya kulitembeza kombe.

Yanga waliofanikiwa kulichukua kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo ikiwa ni mara ya 27 toka kuanz akwa Ligi Kuu Nchini, mabinhwa hao waliambatana namsafara wa viongozi ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Salum Mkemi pampja na benchi la Ufundi.
 Baadhi ya wabunge wakiwa wamelibeba kombe wakionekana kufurahi leo Mkoani  Dodoma.
Baadhi ya wabunge, wachezaji na viongozi wa Yanga wakiwa katika picha ya pamoja leo Mkoani  Dodoma.


MIKAKATI YA WIZARA YA VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI KUUFANYA MKOA WA MTWARA KUWA WA VIWANDA


UVCCM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA HATUA ALIZO CHUKUA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Umoja wa  Vijana wa Chama  Cha Mapinduzi (UVCMM), umenpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk .John Pombe Magufuli kwa kuonesha Uzalendo mkubwa alionao kwa nchi yake,baada ya kuchukua maamuzi yenye maslahi ya nchi  katika sakata la zima la Makinikia.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu mkuu wa  Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  alipokuwa akitoa salamu za pongezi za Vijana wote katika  ukumbi wa CCM vIJANA kinondoni .

Shaka amesema Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi unampongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa   uzalendo wa hali ya juu alionao kwa Taifa mara baada ya kuchukua maamuzi yenye maslahi ya nchi katika swala zima la Makinikia.

Amesema Umoja wa Vijana wa CCM unaunga mkono maamuzi yote yaliyopitishwa au kutolewa na Rais Dk John Magufuli mara baada ya kupokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi 

“Umoja wa Vijana wa CCM hatuko tayari na hatutakubali kushuhudia tena Tanzania  ikirejea katika zama ya kiza kinene cha ukwapuaji mali,  ulaji, kufilisi mashirika ya umma au wizi wa mali za umma,tunaishauri serikali yetu iendelee na mikakati yake ya kuhakikisha ukwapuaji, ubabaishaji, wizi na ufisadi wa mali za serikali vinavikomeshwa mara moja     
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa maamuzi aliyochukua.
 Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwa na Viongozi wa ngazi za juu wa umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Akiwa amebebwa juu  na Vijana wa CCM
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili  katika ukumbi wa Umoja wa Vijana Kinondoni.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


SERIKALI YAWAHIMIZA WANANCHI KUCHANGAMKIA MIFUKO YA UWEZESHAJI KIUCHUMI NCHINI.

Na Daudi Manongi, MAELEZO DODOMA

Serikali kupitia Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) lililopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imewataka wananchi kuitumia vyema mifuko 19 ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kujipatia mitaji yenye riba nafuu.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akijibu maswali mbalimbali ya wabunge leo Mjini Dodoma.

“Serikali inawawezesha wananchi ili waweze kukopesheka kupitia Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004 na Sheria ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi Na.6 ya mwaka 2004, Alisema Mhe.Mavunde.

Amesema Sera hii imeainisha nia ya Serikali ya kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa mitaji kwa kuboresha vyanzo vya akiba na kuchukuwa hatua za kuondoa vikwazo mbalimbali ili kuwezesha mabenki kukopesha kikamilifu amana zilizopo kwa gharama nafuu,kupitia vikundi vidogo,SACCOS na Vicoba.

Aidha kutokana na Sera hii Mipango, Miradi na Mifuko kadhaa imeanzishwa na Serikali ili kuwezesha wananchi kukopa kwa urahisi ambapo katika mifuko hiyo 19 baadhi yake ni pamoja na Mfuko wa kuendeleza wajasirimali wananchi,mfuko wa uwezeshaji wa mwananchi,mfuko wa pembejeo za kilimo,mfuko wa maendeleo ya vijana, mfuko wa dhamana za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati,mfuko wa dhamana za mikopo kwa mauzo ya nje ya nchi ambapo hadi kufikia mwaka 2016 mifuko hii ilikuwa imetoa mikopo ya trilioni 1.7 kwa wajasiriamali 400,000.

Pamoja na hayo Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri kwa vyombo hivyo kuweza kutoa huduma kwa wananchi.

“Serikali kupitia Benki kuu ya Tanzania kulingana na mazingira inaendelea kuangalia viwango vya riba kwa mabenki na Taasisi za fedha ili zimudu kupata fedha zaidi kwa ajili ya kukopesha wajasiriamali kwa riba ndogo,ambapo pia imechukua hatua ya kupunguza kiwango cha riba kwa mikopo yake kutoka asilimia 16 hadi asilimia 12 ”,Alisisitiza Mavunde.


SINGIDAUNITED YANASA SAINI YA KIUNGO WA MBEYA CITY

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kiungo mahiri wa timu ya Mbeya City Kenny  Ally amejiunga rasmi na klabu ya Singida United kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa kandarasi ya miaka miwili.

Kenny ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wakiwindwa vikali na klabu kubwa za hapa nchini Simba na Yanga kila mmoja akitaka kupata saini yake ila walikuwa wakishindwana katika dau.
Usajili huo wa Kenny kwenda  Singida United ni pigo kwa timu ya Mbeya City kwani inaonekana ikiendelea kuvunjwa  kwa kusajiliwa wachezaji wao na klabu mbalimbali.

Singida United ni miongoni mwa timu ambazo zimeanza kutazamwa na wadau wa soka kwamamba huenda wakaleta mapinduzi katika soka hapa nchini hii inatokana na mipango yao ikiwemo usajili wa wachezaji wa kigeni.
 Mchezaji Kenny Ally akipokea jezi yake kutoka kwa Katibu Mkuu wa Singida United Abdulrahman Sima baada ya kukamilisha kutia saini kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia klabu hiyo, katikati ni  Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Singida Festo Sanga.
 Mchezaji Kenny Ally akitia saini kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia klabu hiyo. Kulia ni  Katibu Mkuu wa Singida United Abdulrahman Sima na  Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Singida Festo Sanga.


GHANA NA MALI ZATINGA FAINALI KOMBE LA VIJANA GABON

Timu za vijana za Ghana na Mali zimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17.

Ghana wametinga fainali baada ya kupata ushindi wa penati 6-5 dhidi ya Niger baada ya kwenda sare katika dakika tisini za mchezo.

Mabingwa watetezi Mali wao wamefanikiwa kutinga fainali yao ya pili mfululizo baada ya kuwaondosha Guinea kwa penati 2-0 huku kipa wa Mali Youssouf Koita, akiwa shujaa wa timu hiyo kwa kuokoa michomo mingi na penati.

Mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya vijana utapigwa jumapili ya tarehe 28 mchezo ukichezwa katika dimba la AmitiƩ Sino-Gabonaise, mjini Libreville,

Mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Niger na Guinea nao utafanyika siku hiyo hiyo ya jumapili katika uwanja wa katika uwanja AmitiƩ Sino-Gabonaise.


Vodacom yaongeza bajeti ya zawadi Ligi Kuu mwaka huu


Wadhamini wakuu wa Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, jana ilitoa zawadi zenye thamani ya shilingi 232,974,660 kwa washindi mbali mbali wa ligi.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi Mkuu wa biashara na Masoko wa kampuni hiyo,Hisham Hendi alisema Vodacom imeongeza kiasi cha fedha zaidi mwaka huu.

Mwaka jana tulitoa shilingi 219,502,500. Kwa ajili ya zawadi lakini mwaka huu fedha hizi zimeongezeka na kufikia shilingi 232,974,660,” alisema

Hendi alisema, Vodacom Tanzania inavutiwa na jinsi ambavyo umaarufu wa ligi unavyokuwa ukiongezeka siku hadi siku huku ukiwavutia na kuwaburudisha Watanzania walio wengi wanaoishi mijini na vijijini bila kujali kama timu za maeneo wanayoishi zinashiriki ligi hii.

“Pamoja na umaarufu wa ligi hii kuongezeka na mafanikio yanayozidi kupatikana, sisi kama wadhamini tunajua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali za kuboresha ligi yetu iwe na viwango vya hali ya juu na ili kuondokana na changamoto hizi unahitajika ushirikiano mkubwa baina ya wadau wote wa mchezo wa soka nchini japo mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja,” alieleza.

Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wadau wote kushiriki kubuni mikakati ya kuboresha ligi hii na ikiwezekana wajitokeze wafadhili wengine zaidi ili wachezaji wazidi kunufaika.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(kushoto) wakimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuchukua tuzo hiyo hapo jana wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella, akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 84/- Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa baada ya timu yao kuibika mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (kushoto) akimkabidhi tuzo ya heshima, Kitwana Manara wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) akimshuhudia Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi(kushoto)akimpongeza baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.